Mbunge: Serikali inachukua mgawanyo mkubwa wa viingilio uwanjani

0
31

Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Mtinga ameiomba Serikali kupitia upya mgawanyo wa mapato ya viingilio yanayopatikana uwanjani katika timu za mpira nchini ili kuzipa faida vilabu hivyo.

Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza, Mtinga amedai Serikali inakata makato makubwa sana uwanjani huku akitolea mfano mchezo wa hivi karibuni kati ya Simba na Yanga ambapo Simba ilipata milioni 180 kati ya milioni 450 zilizopatikana katika viingilio.

“Kwa mfano juzi Simba imepata milioni 450 kwenye mchezo [Simba na Yanga] lakini inaambulia 180 makato mengi ambayo hayaeleweki, lini Serikali itapitia upya makato ili kuziokoa timu,” amehoji

Rais Samia apandisha dau magoli ya Simba na Yanga hadi milioni 10

Akijibu swali lake, Naibu Waziri wa Michezo, Hamis Mwinjuma amesema kuna gharama kubwa sana za uendeshaji wa michezo lakini Serikali inaangalia namna bora ya kuviwezesha vilabu kufaidika na michezo hiyo.

“Tunaangalia utaratibu ambao utawezesha vilabu vyetu kunufaika zaidi, lakini kuna gharama kubwa za uendeshaji wa michezo inayotajwa na taasisi zetu zinaingia gharama kubwa ambayo inatoka mifukoni kwao kuweza kuifanya michezo hii ifanikiwe.

Kwa hiyo pamoja na lengo letu la kuhakikisha timu zetu zinafaidika lakini kuna gharama kubwa za uendeshaji na taasisi zetu zitashindwa kujiendesha kama tutazizuia kukata makato yao” amesema.

Send this to a friend