Mbunge wa CCM afariki dunia India

0
37

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla amefariki dunia katika Hospitali ya HCG Mumbai, India alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai imeeleza kuwa Bi. Umbulla amefariki siku ya Alhamisi Januari 21, 2021, saa 7 usiku kwa saa za India.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na wananchi wa Mkoa wa Manyara. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika

Ofisi ya Bunge imesema kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Mwanasiasa huyo alizaliwa Novemba 10, 1955.

Send this to a friend