Mbunge wa Tanzania akutwa na maambukizi ya corona

0
33

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt Tulia Ackson, ametangaza kuwa mmoja wa wabunge wa bunge hilo amethibitika kuwa ana maambukizi ya virusi vya Corona.

Naibu spika ametoa tangazo hilo bungeni mjini Dodoma wakati akiahirisha kikao cha 12 cha bunge la bajeti ambapo pia ametumiwa wasaa huo kuwahimiza wabungeni wengine kuzingatia kanuni zote za afya zilizotolewa ikiwemo kila mbunge kukaa kwenye kiti chake.

“Tumepata taarifa kuwa mmoja wetu tayari amepata maambukizi ya COVID-19. Mgonjwa huyo anaendelea vizuri na Serikali inaendelea kumuangalia na kumpatia matibabu stahiki, na maelezo ya mbunge huyo alisafiri kwenda Dar es Salaam siku za hivi karibuni”, ameeleza Dkt. Ackson.

Ameongeza kuwa mbunge huyo alianza kujisikia vibaya Jumatano iliyopita, na alipofanyiwa vipimo alibainika kuwa na maambukizi ya homa ya mapafu (COVID-19).

Send this to a friend