Mbunge: Wazazi wanawashawishi watoto kufeli ili kuwapunguzia gharama

0
38

Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoani Tanga, Husna Sekiboko amesema baadhi ya wazazi wilayani Lushoto mkoani humo huwashawishi watoto wao wafeli mitihani yao ya darasa la saba ili kuwapunguzia gharama kubwa ya kuwapeleka sekondari.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, amesema wilaya hiyo katika tarafa ya Mlola kuna watoto 1,600 ambao wameshindwa kwenda Sekondari kwa mwaka huu kutokana na kushindwa kufikia kiwango cha ufaulu ambao umechangiwa na ushawishi kutoka kwa baadhi ya wazazi.

Serikali yafunga Wi-Fi ya bure maeneo ya umma

“Hii ni kwa sababu wazazi wamekaa na hawa watoto wakakubaliana wafeli kwa sababu gharama ya kumsomesha huyo mtoto kwenye shule ya kata ni kubwa mno,” amesema.

Aidha, amebainisha kuwa elimu bila malipo inawanufaisha wanafunzi wanaoishi karibu na shule hizo lakini waishio mbali hawafurahii elimu inayotolewa na Serikali, hivyo kupelekea wazazi wilayani humo kutumia gharama kubwa kuwasomesha watoto wao.

Send this to a friend