Mbuyu maarufu Dar hatarini kuondolewa kupisha mradi wa BRT

0
123

Moja ya alama maarufu za Dar es Salaam iko hatarini kuondolewa kutokana na upanuzi unaoendelea wa Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi (BRT).

Mbuyu mkubwa ulioko Mbuyuni katika eneo la Oysterbay upo katikati ya njia inayopendekezwa ya barabara ya mabasi ya mwendo kasi kando ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Mbuyu huo ni wa kale na maarufu kiasi kwamba shule ya msingi na kituo cha mabasi katika eneo hilo vilipewa jina lake.

Ujenzi unaoendelea wa Awamu ya Nne ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi (BRT 4), ambao unachukua umbali wa kilomita 13.5 kutoka Kijazi Bridge (Sam Nujoma) – Mwenge – Maktaba Kuu ya Taifa (Posta), utasababisha kuondolewa kwa mbuyu mkubwa ulioko wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Maandalizi ya kuondoa mbuyu huo tayari yameanza, ambapo alama nyekundu ya X imechorwa katikati ya shina la mti huo.

Chanzo: The Citizen

Send this to a friend