Mbwa 400 wahofiwa kufariki baada ya kula mahindi yenye sumu Zambia

0
19

Serikali nchini Zambia imesema takriban mbwa 400 wanahofiwa kufa mwezi mmoja uliopita nchini humo baada ya kula mahindi yenye sumu na kwamba huenda binadamu wakawa hatarini kudhurika pia.

Waziri wa afya wa nchi hiyo, Elijah Muchima ametangaza kuwa takriban nusu ya sampuli 25 zilizochukuliwa kutoka kwa kampuni za kusaga mahindi zilipatikana kuwa na viwango vya juu sana vya aflatoxin, dutu yenye sumu inayozalishwa na kuvu.

Mahindi ni chakula kikuu nchini Zambia na Muchimi amesema matokeo ya sampuli zilizochukuliwa yanatia wasiwasi mkubwa kutokana na athari nyingi za kiafya kwa [watu].

Shirika la Chakula Duniani (WHO) limesema kuna ushahidi kwamba sumu kuvu inaweza kusababisha saratani ya ini kwa binadamu.

Chanzo: BBC Swahili

Send this to a friend