Mbwa wote wanaozurura mitaani kuuawa Kibaha

0
79

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imeagiza mbwa wasiokuwa na makazi na kuzurura ovyo mitaani kuuawa kwani wamekuwa tishio kubwa kwa jamii kutokana na kuwang’ata watu na kusababisha madhara.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Erasto Makala amesema mbwa wanaozurura mtaani hawana chanjo hivyo wanapowang’ata watu huwaletea madhara makubwa kiafya.

“Madhara ya mtu kung’atwa na mbwa ni makubwa hivyo lazima kuwamaliza mbwa wanaozurura kama hawana mwenyewe kwani hawana chanjo ya kuwakinga na magonjwa,” ameeleza.

Aidha, halmashauri hiyo imesema ifanyike sensa ya wanyama hao ili idadi yake iweze kutambulika na kupatiwa chanjo kwa urahisi, kwa wale wanaofugwa kwa utaratibu unaotambulika rasmi na wa kisheria.