Mbwana Samatta kutimkia Fenerbahçe

0
40

Tetesi za soka zinaeleza kuwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza Mbwana Samatta anahusishwa na uhamisho wa kutimkia klabu ya Fenerbahçe ya nchini Uturuki.

Fenerbahçe ambayo imeanza kupanga kikosi chake kuhakikisha inakuwa imara katika msimu ujao imeonesha nia ya kutaka kumsajili Samatta aliyetua Villa Park mapema Januari mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na 90min.com, Aston Villa imeonesha utayari wa kumruhusu nyota huyo aliyetokea KRC Genk kuondoka.

Samatta alisajiliwa na Aston Villa baada ya kufanya vizuri nchini Ubelgiji lakini tangu ametua nchini Uingereza amekuwa hafanyi vizuri katika klabu hiyo iliyopo katika hati hati za kujinasua isishuke daraja.

Kabla ya kujiunga na Aston Villa kulikuwa na tetesi kuwa nyota huyo alikuwa pia akiwindwa na Fenerbahçe

Inatajwa kuwa thamani ya soko ya Samatta kwa sasa ni takribani shilingi bilioni 26.

Send this to a friend