Mchakato wa kumchagua Papa mpya wa Kanisa Katoliki kuanza Mei 7

0
5

Vatican imesema Baraza la Makardinali wa Kanisa Katoliki linatarajia kuanza kikao chake cha siri Mei 7, 2025 kwa ajili ya kumchagua Papa mpya kufuatia kifo cha Papa Francis Aprili 21, mwaka huu.

Uamuzi wa kuanza kwa mchakato huo umeafikiwa katika kikao cha faragha cha makadinali kilichofanyika Vatican, ikiwa ni kikao cha kwanza kufanyika tangu mazishi ya Papa Francis yaliyofanyika Jumamosi.

Papa mpya huchaguliwa na Makardinali kutoka mataifa mbalimbali wenye umri chini ya miaka 80 ndani ya siku 15 hadi 20 baada ya kifo cha Papa.

Papa Francis alizikwa Jumamosi Aprili 26, 2025 na kuhudhuriwa na takriban                                 watu 400,000 waliomiminika kushuhudia maandamano ya kuelekea eneo lake la mazishi katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu.