Mchechu aishtaki The Citizen, ataka fidia TZS bilioni 3

0
49

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa  (NHC), Nehemiah Mchechu  amelishtaki gazeti la The Citizen katika Mahakama Kuu ya Tanzania akiomba kulipwa fidia ya TZS bilioni 3 kwa madai kuwa liliandika habari zilizomchafua.

Katika kesi hiyo iliyosikilizwa Ijumaa ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam mbele ya jaji Leila Mgonya, alidai kwamba Machi 23, 2018 gazeti hilo lilichapisha habari iliyokuwa na kichwa cha habari kilichosomeka kuwa ‘Why JPM dissolved NHC Board, sacked Mchechu,” kwa tafsiri isiyo rasmi (Kwanini JPM alivunja Bodi ya NHC, kumfukuza Mchechu).

“Machi 23, 2018 ilikuwa siku ya kiza kwangu, ni siku ambayo niliandikwa na gazeti la The Citizen ukurasa wa mbele habari ambayo ililenga kunichafua, kunishushia hadhi, kunikosanisha na jamii kubwa ya Watanzania na kuonekana kuwa ni mtu nisiyefaa kabisa kuwa kiongozi, mtu nisiye na maadilli, nisiyeamika na kimsingi nisiyestahili hata kuongoza popote,” amesema Mchechu.

Aidha, amedai kwamba habari hiyo ina upotoshaji mkubwa kimantiki na kimaudhui kwa kuwa hajawahi kufukuzwa kazi na Hayati John Pombe Magufuli kama habari hiyo ilivyodai wala kujihusisha na tuhuma zote zilizoandikwa.

Wazazi wamshtaki kijao wao kwa kutowapatia mjukuu

Mchechu alirudishwa katika nafasi yake ya uongozi na Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kondoka mwaka 2018.

Kwa mijibu wa habari hiyo, Mchechu anadaiwa kumtumia mkandarasi wa NHC kutengeneza barabara kwenda kwenye eneo lake lililokaribu na eneo la mradi wa Safari City huku gharama zikibebwa na S
shirika.

Pia taarifa hiyo ilidai kuwa kampuni ya PHILS International ya Dubai, ilipewa kazi katika mradi wa Kawe iliyotolewa na Mchechu bila kumhusisha mkuu wa kitengo cha ununuzi cha NHC, Hamis Mpinda pamoja na ukiukwaji mkubwa na matumizi mabaya ya fedha za umma uliyofanywa na Mchechu.

Chanzo:Nipashe

Send this to a friend