Mchekeshaji wa Tiktok alazwa kwa kula buibui

0
34

Mtayarishaji wa maudhui yenye utata nchini Kenya, Aq9ine amejikuta akilazwa hospitalini huku akiwa katika hali mbaya baada ya kudaiwa kula buibui.

Kulingana na chapisho kwenye ukurasa wa Instagram, mtumiaji huyo maarufu Tiktok alilazwa baada ya kifua chake kuanza kuuma na kupata homa kali iliyofikia nyuzi joto 48.

Hayo yamejiri baada ya hivi karibuni kuchapisha video iliyomuonesha uso na mkono wake ukiwa umevimba huku akiwaomba wafuasi wake wamuombee.

Katika video hiyo, alionekana akijikuna uso wake ambao ulionekana kuvimba sana pamoja na mikono iliyojaa upele akieleza kwamba, amepata madhara hayo baada kitendo chake cha kula buibui.

“Jamani fanyeni maombi yenu ya mwisho kabla sijaenda [sifaja]. Mniombe tu bana mi naenda [nakufa]. Nasikia ni kama sina uso, nimefura kila mahali. Nimedishi [nimekula] buibui bana na hili linanitokea usoni mzima,” amesema kwenye video hiyo.

Kijana huyo amewahi kuonekana akila popo, panya na kuwashangaza watuamiaji wa mtandao huo na baada ya tukio hilo baadhi wa Wakenya walimshambulia huku akijibu mapigo kuwa mara atakapo pona atakula chura pamoja na nyoka.

Send this to a friend