Mchengerwa amsimamisha kazi Mkurugenzi Halmashauri ya Busega

0
19

Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busega mkoani Simiyu, Veronica Sayore ili kupisha uchunguzi wa malalamiko dhidi yake.

Mchengerwa amechukuwa uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko kuhusu utendaji kazi usioridhisha, kutokuwa na ushirikiano na viongozi wenzake pamoja na kutowashirikisha watendaji katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Kutokana na tuhuma hizo, Mheshimiwa Waziri Mchengerwa amemwelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuunda timu ya uchunguzi wa mwenendo wa utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo pamoja na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Busega,” imeeleza taarifa.

Aidha, Mchengerwa amewataka wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kusimamia dhana ya ushirikishwaji wa viongozi, watendaji na wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuimarisha mahusiano mazuri baina ya viongozi na watendaji ili kujenga timu yenye umoja katika kutekeleza jukumu la kuwahudumia wananchi.

Send this to a friend