Mchina aliyewatesa wafanyakazi wake jela miaka 20

0
38

Mahakama nchini Rwanda imemhukumu raia wa China Sun Shujun kifungo cha miaka 20 jela baada ya video iliyosambaa ikimuonesha mwanaume huyo akiwachapa wanaume wawili waliokuwa wamefungwa kwenye mti Agosti mwaka jana.

Aidha, mahakama pia imemhukumu raia wa Rwanda, Renzaho Alexis kifungo cha miaka 12 jela kwa kumsaidia kutekeleza uhalifu huo.

Waathiriwa hao ambao walishtumiwa na Shujun kwa madai ya wizi wameripotiwa kuwa wafanyakazi wa zamani katika mgodi unaoendeshwa na Shujun katika wilaya ya Rutsiro nchini humo.

Hata hivyo, Ubalozi wa China nchini Rwanda umekubali uamuzi huo wa mahakama uliotolewa Aprili 19, mwaka huu, na kuwataka raia wa China wanaoishi Rwanda kutii sheria za ndani.

Send this to a friend