Maige Lameck (20) mchunga ng’ombe katika Kata ya Lwamgasa mkoani Geita amejeruhiwa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani baada ya kuvamiwa na wakulima katika eneo hilo wakidai mazao yao kulishwa ng’ombe.
Akizungumza na Swahili Times, Maige amesema alivamiwa na baadhi ya wakulima wakidai ng’ombe wake wamelishwa mazao yao kisha wampiga na kitu chenye ncha kali kichwani na kupelekea kupoteza fahamu.
“Alinipiga nikaona kizunguzungu nikawa naona kama watu wengi yaani sijielewi, nikaanguka nikaona wengine wanakimbia wenzangu hao awamu yao wakasema wewe unakimbia wapi baki hapa leo nawaua sasa mimi nikapata kizunguzungu nikashindwa kunyanyuka,” amesimulia Maige.
Mabasi 750 ya Mwendokasi kupelekwa Mbagala
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Lwamgasa, Emmanuely Alphonce amekiri kuwepo kwa tukio hilo la kujeruhiwa mchungaji huyo, huku ng’ombe zaidi ya 30 wakijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga na wakulima.
Alphonce amesema baada ya kupata taarifa walifika kwenye eneo la tukio na kukuta baadhi ya ng’ombe pamoja na Mchungaji huyo aliyejeruhiwa huku akiwataka wakulima hao kutojichukulia sheria mkononi.