Mchungaji Edwin Taji wa Kanisa la Anglicana, Yombo Kiwalani jijini Dar es Salaam anadaiwa kusimamishwa kutoa huduma ya kichungaji baada ya kudaiwa kumtorosha mke wa muumini wake na kumpangishia nyumba eneo la Pugu Kajiungeni.
Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema madai dhidi ya mchungaji huyo yalitolewa na muumini wa kanisa hilo, Simon Ngalawa mkazi wa Yombo Kiwalani akilalamika kuwa mkewe Ester Makunya anajihusisha kimapenzi na mchungaji Tija.
Sababu 5 kwanini wanaume na wanawake hupeana talaka
Ngalawa anadai baada ya kupata tetesi hizo kutoka kwa waumini na ndugu zake, alibaini kuwa mkewe alianza kuwa na fedha wakati hafanyi kazi wala biashara, na kwamba baada ya kupitia kipindi kigumu cha maisha ndipo alipoondoka nyumbani miaka mitatu iliyopita na kuishi Kiwalani ambako inadaiwa alipangishiwa nyumba na kufunguliwa duka na mchungaji huyo.
Ameongeza kuwa licha ya kuitisha vikao vya familia, kwenda Ustawi wa Jamii na Polisi kweye Dawati la Jinsia, lakini imeshindikana kwa mkewe kurudi nyumbani, na ndipo alipokutana na viongozi wa juu wa kanisa hilo ili kumshitaki mchungaji huyo.
Rai Mwema imedai taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zinaeleza kuwa mchungaji Tija amesimamishwa wiki mbili zilizopita huku shauri lake likiendelea kujadiliwa na wakuu wa kanisa hilo.
Chanzo: Raia Mwema