Mchungaji afariki akijaribu kufunga siku 40 kama Yesu

0
58

Mchungaji mmoja nchini Msumbiji amefariki dunia baada ya kufunga kwa siku 40 bila kula akijaribu kufikia rekodi iliyofikiwa na Yesu Kristo kwenye Mlima wa Mizeituni katika historia ya Biblia.

Kifo cha Francisco Barajah, mchungaji na mwanzilishi wa Kanisa la Kiinjili la Santa Trindade katika jimbo la kati la Manica, kimethibitishwa kutokea Jumatano Februari 15, mwaka huu.

Mpangaji adaiwa kumuua mwenye nyumba kwa madai ya kodi

Inadaiwa kuwa baada ya siku 25 za kufunga, mchungaji huyo alipungua sana uzito wake kiasi cha kushindwa kusimama, kuoga au kutembea, kisha siku chache baadaye ndugu na waumini wake walimsisitiza kupelekwa hospitalini kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Taarifa zinaeleza kuwa jitihada za kumrejesha kwenye afya yake hazikuzaa matunda, kwani umauti ulimkuta wakati akitibiwa katika hospitali ya Beira ambako alihamishiwa akiwa katika hali mbaya.

Send this to a friend