
Mchungaji James Irungu kutoka Murang’a nchini Kenya amekimbizwa hospitali baada ya kuishiwa nguvu na kuanguka wakati akijaribu kuweka rekodi mpya ya dunia ya kukumbatia mti kwa muda mrefu zaidi.
Irungu alianguka baada ya kushindwa kuvumilia uchovu saa moja tu kabla ya kukamilisha lengo lake la kukumbatia mti kwa saa 80.
Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Kaunti ya Murang’a anayeshughulikia Masuala ya Vijana, Manoah Gachucha, hali ya mchungaji huyo ni shwari.
“Kwa sasa Mchungaji Jimmy Irungu yupo Hospitali ya Murang’a Level Five akifanyiwa vipimo vya afya. Viungo vyake muhimu viko sawa; tatizo ni uchovu tu, na anapatiwa huduma stahiki na timu yetu ya madaktari,” ameema Gachucha.
Mwanaharakati wa mazingira kutoka Kenya, Truphena Muthoni aliweka rekodi ya kukumbatia mti kwa muda mrefu, ambapo alifanikiwa kutimiza ‘challenge’ ya kukumbatia mti kwa saa 48.







