Mchungaji anayesakwa na FBI kwa biashara ya ngono kwa watoto akamatwa

0
10

Mchungaji wa Ufilipino, Apollo Quiboloy mwenye ushawishi mkubwa na aliyekuwa akisakwa nchini Ufilipino na Marekani kwa tuhuma za biashara ya ngono kwa watoto na usafirishaji haramu wa binadamu amekamatwa Ufilipino.

Apollo ambaye kanisa lake la Kingdom of Jesus Christ (KOJC) linadaiwa kuwa na wafuasi milioni saba, amekanusha mashtaka yote dhidi yake huku akisema kuwa madai hayo ni sehemu ya mapambano ya kuwa Mwana wa Mungu aliyeteuliwa.

Mwaka 2021, Idara ya Haki ya Marekani (DOJ) ilimshtaki kwa ulanguzi wa watoto, ulaghai na ulanguzi wafedha, huku Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) likisema kuwa alisafirisha wasichana na wanawake kutoka Ufilipino hadi Marekani, ambako walilazimishwa kuomba fedha kwa ajili ya shirika ghushi la kutoa misaada.

Hata hivyo, Mamlaka za Ufilipino hivi karibuni pia zilimshtaki kwa unyanyasaji wa watoto, unyanyasaji wa kijinsia na biashara ya binadamu, na hati ya kukamatwa kwake ilitolewa.

Kukamatwa kwa Apollo kunakuja baada ya wiki mbili za misuguano na mapigano ya hapa na pale kati ya polisi na wafuasi wa mchungaji huyo, huku muumini mmoja akipoteza maisha kutokana na mshtuko wa moyo.

Send this to a friend