Mchungaji azikwa baada ya familia kusubiri afufuke kwa siku 600

0
45

Baada ya takribani siku 600 za kungoja ufufuo ambao haujawahi kutokea, mchungaji kutoka Afrika Kusini, Siva Moodley amezikwa kwa heshima katika makaburi ya Westpark huko Johannesburg.

Moodley ambaye ni mwanzilishi wa kanisa la ‘The Miracle Center’ Kaskazini mwa Johannesburg, alifariki Agosti 15, 2021, familia yake ikahifadhi mwili wake kwenye chumba cha kuhifadhia maiti wakiamini kwamba angefufuka.

Meneja wa nyumba ya kuhifadhia maiti, Martin du Toit alilazimika kupata amri ya mahakama ya kuzikwa kwa mwili wa mchungaji huyo baada ya familia ya Moodley kutouchukua au kutoa kibali cha kuzikwa au kuchomwa.

Anusurika kifo baada ya kumeza pete ya uchumba iliyofichwa kwenye chakula

Ripoti zinasema, Martin alijaribu mara 28 kuwasiliana na mke wa Moodley na watoto wake, huku mkewe akidai alikuwa na maono kwamba mumewe anaweza kufufuka, ambaye alikuwa akihubiri katika uhai wake kwamba “mkristo yeyote asife kwa ugonjwa.”

Tangu kifo cha Moodley, ibada katika kanisa hilo zimekuwa zikiendelea kama kawaida zikiendeshwa na mkewe, Jessie na wanae.

Hata hivyo, kanisa hilo limedaiwa kutokiri wazi kifo chake kwenye mitandao ya kijamii au kuwafahamisha waumini mahali alipo, huku jumbe kwenye mitandao yake ya kijamii hasa Facebook na Twitter zikitumwa kila siku kana kwamba zinatoka kwake.

Send this to a friend