Mchungaji jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi

0
50

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Chalinze Dayosisi ya Morogoro, Boniface Mgalula amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani imemtia hatiani mtuhumiwa huyo katika makosa mawili yaliyokuwa yakimkabili baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa.

Marufuku ulaji nyama ya nguruwe

Mchungaji huyo anadaiwa kufanya kosa hilo Januari 6, 2020 huko Chalinze Wilaya ya Bagamoyo, ambapo mtuhumiwa alimbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 16.

Aidha, Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Pwani, Joyce Mushi amesema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ni upande wa mlalamikaji pamoja na kipimo cha vinasaba (DNA) ambacho kilithibitisha kwa asilimia 99.9 kwamba mtoto aliyezaliwa na mwanafunzi huyo ni wa Mchungaji Mgalula.

Send this to a friend