Mchungaji kortini kwa tuhuma za kutapeli bilioni 1.6

0
46

Mchungaji wa Kanisa la Reviva Assemblies of God, Joram Kaminyonge (47) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo kujipatia TZS bilioni 1.6 kwa njia ya udanganyifu.

Inadaiwa mtuhumiwa alijipatia kiasi hicho cha pesa kutoka Kenya Commercial Bank Tanzania Limited akijifanya kwamba Zainabu Kasakwa amekubali kumdhamini mkopo huo jambo ambalo si kweli.

Muuguzi afikishwa mahakamani kwa kumlawiti mgonjwa

Aidha, katika shitaka la pili la utakatishaji fedha ilidaiwa katika tarehe na neo hilo mshtakiwa alijipatia kiasi hicho cha fedha wakati akijua ni zao la kosa tangulizi la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo, mtuhumiwa alikana mashitaka hayo huku kesi ikipangwa kusikilizwa tena Novemba 2 mwaka huu na mtuhumiwa kurudishwa mahabusu.

Send this to a friend