Mchungaji kutoka DR Congo aondolewa nchini kwa mara ya tatu

0
48

Idara ya uhamiaji nchini kwa kushiriana na Ubalozi Mdogo wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliopo mkoani Kigoma, imemrejesha kwao raia wa Congo, Askofu Mkombo Muyondi kwa kosa la kuingia nchini bila kufuata sheria.

Msemaji wa Idara hiyo, Si Paul Mselle amesema Askofu huyo wa kanisa la House of Players Shield of Faith Christian Fellowship lilipo Boco Magengeni Dar es salaam, amerejeshwa kwao kwa mara ya tatu baada ya kufukuzwa kwa mara ya kwanza 2011 kwa tuhuma za kuingia na kujishughulisha na masuala ya dini bila kibali.

Diwani aliyepotea siku tatu akutwa kwa mwanamke Tabata 

Mselle amesema Askofu Muyondi ni mhamiaji haramu ambaye hatakiwi kuingia na kufanya shughuli yoyote hapa nchini mpaka hapo amri ya kufukuzwa kwake ya mwaka 2011 itakapofutwa.

Kufuatia hatua hiyo, Mselle ametoa wito kwa Watanzania kutompokea tena kiongozi huyo kwenye maeneo yao ama kushirikiana naye katika shughuli yoyote mpaka hapo zuio lake litakapofutwa.

Send this to a friend