Mchungaji Msigwa awataka vijana wa CHADEMA kuacha matusi mitandaoni

0
72

Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa umewataka wanachama wa chama hicho kuacha kutukanana katika mitandao ya kijamii, badala yake kuvumiliana.

Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa akizungumza katika mkutano maalumu wa chama Wilaya ya Mbeya Vijijini amesema, vijana wengi wamekuwa wakitoa matusi katika mitandao ya kijamii na kuonesha picha mbaya kwa chama.

Taarifa rasmi ya Serikali kuhusu ugonjwa uliozuka mkoani Lindi

Msigwa amesema CHADEMA imekuwa ikijipambanua kwa wananchi kuwa ndicho chama mbadala wa Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini kutokana na matusi yanayotolewa kutoka kwa vijana wa chama hicho, yamekuwa yakionesha utovu wa nidhamu.

“Tunaposema sisi ni bora kuliko CCM, ni lazima tuoneshe kuwa ni wasafi, sasa kuna baadhi ya vijana wanatukana matusi mitandaoni na wakati mwingine wanawatukana hata viongozi, hivyo tabia hii naomba iishe,” amesema.

Msigwa amesisitiza kuwa chama hicho kina wasemaji wakuu ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kukijenga, lakini baadhi ya wanachama wamekuwa wakisema kama vile wao ndio wasemaji wa chama hicho na kuwaonya kuacha tabia hiyo mara moja.

Send this to a friend