MCT: Hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini imeimarika

0
23

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limesema hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini imeimarika ikilinganishwa na miaka iliyopita.

MCT imesema kuanzia Januari hadi Julai 2022 imerekodi matukio 10 ya ukiukwaji wa haki za waandishi wa habari ambazo wamekutana nazo, tofauti na matukio 14 mwaka 2021 na matukio 43 katika kipindi cha mwaka 2020.

“Kwa MCT, ishara ya kwanza kwamba mabadiliko yanakuja ilikuwa utayari wa mawaziri kufanya maongezi na wadau, ambapo wakati wa utawala uliopita baraza lilihangaika bila mafanikio kwa muda wa miaka mitatu kupata nafasi ya kukutana na Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni bila mafanikio wala barua kujibiwa,” imeandika MCT.

Katika taarifa hiyo, imesema katika kipindi cha miezi mitatu cha utawala wa Rais Samia Suluhu, Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) ulikuwa umekutana na waziri wa iliyokuwa Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Waziri wa Katiba na Sheria ili kujadili mfumo wa kisheria unaoongoza vyombo vya habari.

Send this to a friend