Mdee na wenzake wakata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu

0
42

Wabunge 19 wa viti maalum waliovuliwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na Halima Mdee na wenzake wamefika Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kubariki uamuzi wa Kamati Kuu kuwavua uanachama.

Kupitia jopo la mawakili wa wabunge hao, Ipilinga Panya, Aliko Mwamanenge, Emmanuel Ukashu na Edson Kilatu wamewasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa mahakamani kupinga uamuzi huo ambapo baada ya hatua hiyo sasa wanasubiri kupata nyaraka za kesi hiyo ukiwamo mwenendo katika ngazi ya Mahakama Kuu, uamuzi na vielelezo vingine ili waweze kuwasilisha sababu za rufaa.

Kamati Kuu ya CHADEMA iliwavua uanachama Novemba 27, 2020 ambapo wabunge hao walikata rufaa Baraza Kuu kupinga uamuzi huo lakini Baraza hilo katika uamuzi uliofanywa Mei 11, 2022 lilitupilia mbali rufaa hiyo.

Hata hivyo, Mdee na wenzake walifungua kesi Mahakama Kuu, Masijala Kuu wakipinga kufukuzwa uanachama na kupinga uamuzi wa Baraza Kuu kutupilia mbali rufaa zao za kupinga kufukuzwa uanachama.

Send this to a friend