Mdee na wenzake wakata rufaa mahakamani, bunge lashindwa kutoa uamuzi

1
41

Kufuatia sakata la wabunge 19 waliovuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema kwa sasa hawezi kutamka kuwa viti 19 vya wabunge hao vipo wazi kwa kuwa suala hilo lipo mahakamani.

Akizungumza hayo Bungeni jijini Dodoma, Dkt. Tulia amesema alipokea barua kutoka kwa wabunge hao 19 wakimtaarifu kuwa tayari wamefungua shauri mahakamani kupinga kufukuzwa uanachama.

Aidha, ameeleza kuwa Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa mahakama na badala yake linalazimika kusubiri hadi hapo itakapotoa uamuzi wake, kwani mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki ni mahakama.

Awali, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika aliwasilisha barua kwa Spika wa Bunge kumtaarifu kuhusu kutupiliwa mbali rufaa ya wabunge hao, ili aendelee na taratibu nyingine.

Send this to a friend