Mdororo Ethiopia, reli iliyojengwa na China ikihitaji maboresho ya bilioni 141

0
33

Mtandao wa usafirishaji wa reli ya umeme uliojengwa na China katika mji mkuu wa Ethiopia uko mbioni kuporomoka, kutokana na treni zake kuhitaji marekebisho yatakayogharimu zaidi ya dola milioni 60 [TZS bilioni 141.7].

Inaelezwa kuwa, ni treni nane tu kati ya treni 41 zinazofanya kazi katika kipindi cha miaka saba baada ya kuzinduliwa, hivyo matengenezo hayo yanatarajiwa kufanywa na wahandisi walioletwa kutoka China.

Njia ya reli ya kisasa yenye urefu wa kilomita 32, ambayo inaunganisha katikati mwa Addis Ababa na vitongoji vyake ilifadhiliwa na Benki ya China Export-Import na ilianza kufanya kazi mnamo Novemba 2015.

Mwishoni mwa mwaka jana, Benki ya Exim ya China ilizuia mkopo wa zaidi ya dola milioni 339 [TZS bilioni 800] kwa Ethiopia kutokana na Taifa hilo kutokuwa na uwezo wa kulipa mikopo yake ya miundombinu inayoongezeka, huku miradi mingi ikisitishwa kutokana na uhaba wa fedha za kigeni na migogoro ya mara kwa mara.

China ni mkopeshaji mkuu wa Ethiopia ambapo inadaiwa zaidi ya dola bilioni 13 [TZS Trilioni 30.7] . Mnamo Januari 2023, China ilitia saini ya makubaliano ya kusamehe sehemu ya deni la Ethiopia.

Send this to a friend