Mechi ya Simba na Yanga yaingiza milioni 410

0
51

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa Aprili 16, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam imeingiza jumla ya TZS milioni 410.64.

TFF imeeleza kuwa katika mchezo huo jumla ya mashabiki 53,569 waliingia ambapo VIP A waliingia watazamaji 340 kwa kiingilio cha TZS 30,000 na kupatikana jumla ya TZS milioni 10.2 na upande wa VIP B, waliingia watazamaji 4,160 kwa kiingilio cha TZS 20,000 na kupatikana jumla ya TZS milioni 83.2.

Umri halisi wa wachezaji wote wa Simba na Yanga

VIP C waliingia watazamaji 2,004 kwa kiingilio cha TZS 15,000 na kupatikana TZS milioni 30.06, wakati jukwaa la rangi ya machungwa waliingia watazamaji 10,372 kwa kiingili cha TZS 10,000 na kupatikana jumla TZS milioni 103.72, jukwaa la mzunguko waliingia watazamaji 36,693 kwa kiingilio cha TZS 5,000 na kupatikana jumla ya TZS milioni 183.465.

Simba kama timu mwenyeji kwenye mchezo huo imepewa TZS milioni 188.9.

Mchezo huo ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 yaliyofungwa na Henock Inonga na Kibu Denis.

Send this to a friend