Membe ammwagia sifa Rais Samia, ajitolea kumsaidia

0
41

Aliyekuwa mgombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe amesema kuwa anaunga mkono utendaji kazi wa za Rais Samia Suluhu Hassan.

Membe ambaye amewahi kuwa Wizari wa Mambo ya Nje wa Tanzania amesema kuwa anachofanya Rais Samia ni kazi kubwa na nzuri ya kuingoza nchini na kwamba wakazi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla wanafurahia.

Mwanasiasa huyo amebainisha hayo katika ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye yupo mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi.

Akizungumza Membe amesema kuwa yupo tayari kuwa meneja kampeni wa Rais Samia Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Ameongeza kuwa yuko tayari kurejea nyumbani ila anachosubiri ni hukumu ya kesi inayomkabili inayotarajiwa kutolewa hukumu October 12 mwaka huu.

Membe alijiunga na ACT-Wazalendo Julai 15, 2020 na aligombea Urais wa JMT kupitia chama hicho akaibuka na kura 81,129 sawa na 0.5% ya kura zote. Februari 28, 2020 alifukuzwa uanachama wa CCM na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Mwanasiasa huyo alijitoa ACT Wazalendo Januari Mosi mwaka huu, na kwa muda wote huo hajatangaza kama amejiunga na chama chochote.

Send this to a friend