Membe: Nilisimamisha kampeni kutokana na msaidizi wangu kukamatwa

0
39

Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe amesema kuwa kukamatwa kwa msaidizi wake ndiyo sababu iliyompelekea yeye kusitisha kufanya kampeni za uchaguzi.

Membe amesema hayo leo wakati akizungumzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu hatima ya ushriki wake katika uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Mwanadiplomasia huyo amesema asingeweza kuendelea na kampeni zake wakati msaidizi wake amekamatwa na kutuhumiwa kwa kosa la utakatishaji fedha, shitaka ambalo linamhusu yeye kama mgombea moja kwa moja.

“Niliporejea kutoka Dubai… msaidizi wangu mmoja akamatwa kwa tuhuma za utakatishaji fedha… hata wewe ungekuwa mimi, ungesitisha kila kitu kutatua suala ambalo in fact [kiukweli] halikuwepo na lilikuwa linavunja credibility [kuaminika] kwa mgombea.”

Membe amesema kuwa hakutaka kuwa mjinga kumuacha msaidizi wake amekamatwa halafu yeye achanje mbuga kuendelea na kampeni, kwani pia alitumia muda huo kusawazisha kauli tata zilizokuwa zinamkabili.

Jerome Luanda alikamatwa Septemba 2020 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati mgombea huyo aliporejea nchini kutoka Dubai.

Aidha, Membe ameahidi kutumia siku zilizobaki kuendelea na kampeni na kusisistiza kwamba yeye ni mgombea halali wa ACT-Wazalendo.

Send this to a friend