Membe: Sababu zilizoniondoa CCM hazipo tena

0
38

“Nimerejea CCM kwa sababu kuu mbili, sababu ya kwanza nilishauriwa na viongozi wa dini zote, nilishauriwa na viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya na Mkoa, nilishauriwa na marafiki zangu wote nirejee CCM, nilishauriwa na wana CCM.”

Amesema mwanasiasa Bernard Membe akipokelewa tena ndani ya Chama cha Mapinduzi baada ya kuondoka na kugombea Urais kupitia ACT Wazalendo mwaka 2020.

Amesema sababu ya pili ya kurudi kwenye Chama hicho inatokana na dhamira yake ya kukitumikia Chama Cha Mapinduzi hadi atakapokwenda kaburini. “Nilipoondolewa CCM nilisikitika sana, nilisonekana sana, na ninyi wananchi msikitika, mlisononekana.

Akijibu swali kwanini anarudi CCM sasa amesema, “narudi sababu zilizoniondoa CCM haziko tena. Nimerudi, namshukuru Mwenyekiti wa CCM na wajumbe wa Kamati Kuu  kunirudisha. Nimerudi kwenye chama ambacho nimezaliwa na kukulia, chama ambacho kimenisomesha.”

Aidha, akitoa ahadi yake amesema hataondoka tena, atabakia CCM hadi mwisho wa uhai wake. “Sasa Mtama mtakuwa na wabunge wawili, Mbunge wetu Nape na mimi mbunge wa chini chini

Send this to a friend