Meridianbet Waishika Mkono Hospitali ya Madale kwa Kuwapa Vifaa

0
53

 

Dar-es salaam: Kampuni ya Meridianbet Tanzania, Jumatatu hii tarehe 26 Septemba 2022, walitembelea hospitali ya Madale na kutoa vifaa vya usafi na vifaa tiba katika hospitali ya hiyo ambayo inapatikana Tegeta, Kata ya Wazo.

Timu ya Meridianbet ilifunga safari hadi hospitali hiyo, ikiongozwa na Twaha Ibrahim ambaye ni Afisa Masoko wa Kampuni. Timu hii ilikaribishwa na Serikali ya  Mtaa pamoja na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo.

Timu hiyo kutoka Kampuni bora ya ubashiri Tanzania Meridianbet, iliona umuhimu wa kutoa vifaa hivyo katika hospitali hiyo ili kuunga mkono jitihada za kuweka mazingira kuwa safi. Hospitali hii inatoa huduma kwa wananchi wengi uhitaji mkubwa wa huduma za matibabu kutoka maeneo mbalimbali yanayoizunguka Madale.

Diwani wa Kata hiyo Leonard Manyama, ameishukuru kampuni ya Meridianbet kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitaisaidia hospitali hiyo kwenye shughuli za usafi, na pia akaishauri Meridiabet kuwa kitendo hicho kiwe endelevu na kisiishie hapo, na kuwaalika wadau wengine kuunga mkono jitihada kama hizo.

Kaulimbiu inasema “Tunza mazingira yakutunze”. Vilevile usafi huepusha kuleta magonjwa mbalimbali ikiwemo U.T.I, Kipindupindu na mengineyo na Kampuni hiyo maarufu Tanzania inaamini kuwa kwa kidogo hicho ambacho wamekitoa kitaenda kuleta kuisaida vyema jamii nzima.

Meridianbet wametoa vifaa hivyo kwa nia ya kurejesha katika jamii kwa kile ambacho wanakipata kwani “Kutoa ni moyo na si utajiri”. Vifaa ambavyo vimetolewa katika hospitali hiyo ni pamoja na sabuni za kunawia mikono, Glavu za tiba, ndoo za kudekia, mifagio, ndoo za kuwekea taka, pamoja na Disinfectant ambavyo vilikabidhiwa kwa Diwani wa Kata hiyo Leonard Manyama.

Meridianbet, ambao ni mabingwa na wakongwe wa uendeshaji wa michezo ya kubahatisha Tanzania, wakiwa na ubashiri wa michezo na kasino ya mtandaoni, wanasema kuwa hii ni namna bora kwao kuwa karibu na jamii yao.  Meridianbet wanakualika kuendelea kufurahia ubashiri mtandaoni au kupiga *149*10# ukiwa na mtandao wa Airtel au Tigo.

 

 

 

Send this to a friend