Messi atangaza fainali ya Kombe la Dunia kuwa mchezo wake wa mwisho

0
37

Nahodha wa Argentina Lionel Messi (35) amesema fainali ya Jumapili ndiyo utakuwa mchezo wake wa mwisho wa Kombe la Dunia maishani mwake.

Mshambuliaji huyo ambaye alifunga bao lake la tano nchini Qatar na kusaidia kutengeneza magoli mengine mawili yaliyoipa Argentina ushindi wa 3-0 dhidi ya Croatia.

“Nina furaha sana kwa kumaliza safari yangu katika Kombe la Dunia katika fainali, kila kitu nilichokiishi katika Kombe hili la Dunia kimekuwa cha hisia, nikiona jinsi kilivyofurahiwa huko Argentina,” amesema Messi.

Mchengerwa: Tunachunguza sakata la Mwakinyo kupoteza pambano Uingereza

Argentina itacheza na Ufaransa au Morocco, ambazo zitakutana Jumatano katika fainali, wakati mchezaji huyo anayechezea miamba ya Ufaransa, Paris St-Germain (PSG) akitarajiwa kuweka rekodi ya kucheza mechi 26 za Kombe la Dunia.

Kwa sasa anaongoza mbio za kiatu cha dhahabu nchini Qatar pamoja na Mfaransa, Kylian Mbappe, akiwa mchezaji wa kwanza wa Argentina kufunga katika michuano minne ya Kombe la Dunia, pia kuwa mfungaji bora wa Argentina kwenye Kombe la Dunia akiwa na magoli 11.

Send this to a friend