Mexico yasitisha kumpeleka mtoto wa El Chapo nchini Marekani baada ya watu 29 kuuawa

0
47

Jaji kutoka Mexico City amesitisha zoezi la kumpeleka nchini Marekani Joaquín ‘El Chapo’ Guzmán, ambaye ni mtoto wa mfanyabiashara mkubwa wa dawa za kulevya, siku moja baada ya watu 29 kufariki katika operesheni kali zilizofuatia kukamatwa kwake.

Ovidio Guzman, (32) amekamatwa na wanajeshi katika jimbo lake la Sinaloa na kulepelekwa Mexico City kwa helikopta ambapo hivi sasa yuko rumande katika gereza la shirikisho lenye ulinzi mkali.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inataka apelekwe nchini Marekani na imetangaza zawadi ya dola milioni 5 [TZS bilioni 11.7] kwa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwake ambapo wamesema ni mwanachama mwandamizi wa genge la uhalifu la Sinaloa (Sinaloa Cartel).

Mbali na kusitisha uhamisho huo, jaji wa shirikisho mnamo Ijumaa pia alipiga marufuku Guzman kuwasiliana na timu yake ya kisheria na familia, kulingana na taarifa ya CNN.

Siku ya Alhamisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico, Marcelo Ebrard alithibitisha kwamba kuna hati ya kukamatwa nchini Marekani ya Septemba 19, 2019, lakini akasema uwezekano wa kurejeshwa kwa Guzmán hautakuwa wa haraka kwa sababu ya taratibu za sheria na pia Guzmán ana taratibu za kisheria zinazoendelea nchini Mexico.

Baba yake, El Chapo Guzmán aliwahi kutoroka kutoka gereza la Altiplano mnamo Julai 11, 2015 kupitia mtaro wa maili moja. Baadaye alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Marekani kwa makosa 10, ikiwa ni pamoja na kujihusisha na biashara ya uhalifu, ulanguzi wa dawa za kulevya na mashtaka ya kutumia silaha.

Send this to a friend