Meya aliyetenguliwa arudi kugombea tena, adai Moshi imepoa

0
41

Aliyekuwa wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Juma Raibu aliyevuliwa wadhifa huo baada ya kupigiwa kura na madiwani za kukataliwa, amechukua  fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania tena nafasi hiyo.
 
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu katika ofisi za  CCM Moshi Mjini, Raibu amesema ameamua kurudi kuwania nafasi hiyo baada ya kuona kuwa toka ameondolewa kwenye nafasi hiyo Moshi imepoa na haijachangamka kama alivyokuwa kwenye nafasi hiyo.
 
 Amesema zaidi wananchi 500 walifika nyumbani kwake kumuomba na kumchangia ili aweze kurudi kugombea nafasi hiyo.
 
Juma Raibu aling’olewa katika wadhifa huo Aprili 11 mwaka huu baada ya kutuhumiwa kuwa na matumizi mabaya ya ofisi, kujihusisha na vitendo vya rushwa, kuruhusu ujenzi holela na kutumia fedha nje ya utaratibu.
 

Send this to a friend