Meya Mwanza akanusha wananchi wa milimani kuondolewa

0
44

Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine amesema hakuna mwananchi yeyote atakayeondolewa katika maeneo ya milimani hususani maeneo ya Isamilo na Igogo kama ambavyo taarifa zinaenezwa, na badala yake Serikali imeanza kutoa leseni za makazi kwa wananchi hao.

Akizungumza na vyombo vya habari Costantine amesema ni kweli wawekezaji walifika jijini hapo na kuonyesha nia ya kutaka kuwekeza lakini sio kwamba walikwenda kwa ajili ya kuwekeza moja kwa moja.

“Kwa kuwa ilikuwa ni hatua za mwanzo za mazungumzo hayo, tukasema kwamba bado wananchi walikuwa na wigo mpana kwa ajili ya maamuzi hayo na kufanya utaratibu mzima kwa ajili ya ukamilishaji wa hatua kama hizo zilizokusudiwa kwa ajili ya uwekezaji,” amesema Costantine

Aidha, ameongeza kuwa bado Serikali inapokea wawekezaji wakubwa kwa ajili ya kuwekeza na si maeneo ya milimani pekee bali wamekuwa wakijielekeza katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Hata hivyo ametoa rai kwa wananchi na kuwasihi kuondoa hofu katika suala hilo, kwani taratibu zinawaruhusu wananchi kushiriki kwa asilimia kubwa kwenye mipango ya maendeleo katika jiji la Mwanza.

Send this to a friend