Mfahamu Mtanzania Abdulrazak Gurnah aliyeshinda tuzo ya Nobel ya Fasihi

0
62

Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka 2021 imetolewa kwa Mtanzania, Abdulrazak Gurnah kujituma kwake kupitia machapisho yake yanaloelezea athari za ukoloni za madhila yawakumbayo wakimbizi.

Abdulrazak Gurnah ambaye ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hiyo alizaliwa Zanzibar mwaka 1948 lakini alihamia Uingereza akiwa na umri mdogo. Ni mtunzi mahiri wa riwaya ambapo hadi sasa ameandika riwaya 10, nyingi kati ya hizo zinaangazia masiha na changamoto zinazowakumba wakimbizi.

Mwaka 1994 riwaya yake ya Paradise ambayo inaelezea maisha ya kijana aliyekulia Tanzania mapema karne ya 20 ilishinda tuzo ya Booker Prize na kufungua utambulisho wake kama mwanariwaya.

Kabla ya kustaafu, Gurnah ambaye ana miaka 73 alikuwa profesa wa Kiingereza na fahisi baada ya ukoloni (Postcolonial Litereatures) katika Chuo Kikuu cha Kent nchini Uingereza.

Mara ya mwisho mwandishi mwenye asili ya Afrika kutunukiwa tuzo hiyo ilikuwa mwaka 1986 ambayo ilikwenda kwa Wole Soyinka kutoka Nigeria.

Ushindi huo unaambatana na zawadi ya TZS bilioni 2.6. Tunzo hiyo hutolewa kwa mtu ambaye atakuwa amechapisha kazi bora zaidi ya fahisi katika mrengo madhubuti.

Send this to a friend