Mfalme Charles III wa Uingereza kuzuru Kenya

0
75

Mfalme wa Uingereza, Charles III anatarajiwa kuzuru Kenya mwaka huu kama sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano na mataifa ya Jumuiya ya Madola kote ulimwenguni.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya Uingereza, mfalme huyo atazuru nchi hiyo kabla ya kuelekea Ufaransa, safari ambayo ilikuwa ifanyike Machi lakini ikakatishwa kwa sababu ya usalama.

Mkuu wa Jeshi Sudan afungia akaunti za benki za jeshi la akiba RSF

Hii itakuwa ziara ya tano ya Mfalme Charles nchini Kenya na safari yake ya kwanza kama mfalme tangu kutawazwa kwake katika Kanisa la Westminster Abbey mjini London wiki mbili zilizopita.

Kenya inamkumbuka mama yake, Malkia Elizabeth II ambaye alipokea taarifa za kifo cha baba yake alipokuwa nchini humo mnamo Februari 1952 kisha kutawazwa kama Malkia alipokuwa na umri wa miaka 25.

Send this to a friend