Mfalme wa Hifadhi ya Serengeti ‘Bob Junior’ auawa

0
19

Simba anayefahamika kama mfalme wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, maarufu kwa jina la ‘Bob Junior’ ameuawa baada ya kushambuliwa na kundi la Simba watatu wanaodaiwa kuwa na lengo la muda mrefu la kuuangusha utawala wake.

Mamlaka za hifadhi imethibitisha kifo hicho kilichotokea Jumamosi na kueleza kuwa simba huyo anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 10 hakufanya vita alipokuwa akishambuliwa.

Simba ‘Bob Junior’ akisaidiana na kaka yake, Joel walitawala kwa zaidi ya miaka mitano na kuwa miongoni mwa Simba waliotawala kwa kipindi kirefu zaidi kabla ya kufanyika mapinduzi hayo.

“Kwa kawaida hatuwezi kuingilia maisha ya wanyama pori [..] hivyo kilichotokea kilipangwa miongoni mwao ikiwa ni vita vya kimapinduzi na simba huwa wana tabia hiyo ambapo mtawala anapozeeka hutolewa kimabavu,” ameiambia BBC mmoja wa maafisa wa uhifadhi wa mbuga hiyo, Fredy Shirima.

Ndege mpya ya mizigo kuwasili nchini muda wowote

Simba huyo amejibebea umaarufu kwa sifa yake ya upole na mtulivu anapoona watalii, pia ndiye simba mwenye manyoya mengi zaidi na wa kuvutia lakini kubwa zaidi hutulia pale anapopigwa picha.

Wadau wa utalii wamesikitishwa na kifo cha simba huyo huku mamlaka ikiendelea kufuatillia mahali alipo kaka wa Bob Junior, Joel anayedaiwa kuuawa kwa kushambuliwa na washirika wa simba waliomuua Bob Junior.

Send this to a friend