Mfanyabiashara Taalib Mbowe akamatwa kwa tuhuma za utakatishaji fedha

0
17

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inamshikilia kwa mahojiano mfanyabiashara na mmiliki wa Kampuni ya White Star Investiment ya jijini Dar es Salaam.

Mfanyabishara huyo Taalib Mbowe ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo inayojishughulisha na usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi anachunguzwa kwa tuhuma za makosa ya ukwepaji kodi, udanganyifu na utakatishaji fedha haramu.

TAKUKURU pia inachunguza umiliki wa vichwa vya malori zaidi ya 100 vinavyomilikiwa na mfanyabiashara huyo pamoja na mikopo yake ya TZS 6.3 bilioni kutoka Benki ya Barclays na TZS 1.1 bilioni kutoka Benki ya Equity.

Taasisi hiyo imesema kuwa uchunguzi ukikamili na kuthibitisha tuhuma hizo, Mbowe atachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani.

Send this to a friend