Mfanyakazi kiwanda cha pombe ashikiliwa kwa kumuua mpenzi wake Goba

0
149

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemweka chini ya ulinzi mwanaume aliyefahamika kwa jina la Musa Sasi (32) anayefanya kazi ya kibarua katika kiwanda cha pombe ya banana kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake Lucy Haule (29), mfanyakazi wa kiwanda cha pombe kali iitwayo nguvu banana wine.

Katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi kwa vyombo vya habari, imesema leo Julai 25, 2024 ilipokea taarifa kuhusu kutokea kwa tukio hilo eneo la Goba Matosa, Kinondoni Dar es Salaam linalodaiwa kusababishwa na ugomvi kati ya watu wanaodaiwa kuwa ni wapenzi.

“Baada ya kumuua mpenzi wake, mtuhumiwa naye alijaribu kujiua kwa kutumia kisu kwa kujichoma shingoni. Mtuhumiwa huyo amekamatwa na hali yake ni mbaya na yupo Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala,” imeeza taarifa.

Jeshi la Polisi limesema mpaka sasa bado haijulikani chanzo halisi cha ugomvi uliopelekea mauaji hayo, hivyo uchunguzi wa kina bado unaendelea.

Send this to a friend