Dada wa kazi akutwa amejinyonga Musoma

0
36

Mfanyakazi wa ndani aliyefahamika kwa jina moja la Modesta (17) amefariki dunia baada ya kujinyonga Desemba 10, mwaka huu, Mtaa wa Zanzibar katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Pius Lutumo amesema mwili wa binti huyo ulikutwa ukiwa unaning’inia kwenye chumba alimokuwa akilala binti huyo enzi za uhai wake huku chanzo cha tukio hilo kikihusishwa na msongo wa mawazo.

“Huyu binti alikutwa amefariki kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya kufungia mbuzi na mwili wake ulikutwa ukiwa umening’inia kwenye kenchi la paa ya chumba chake,” amesema.

Aidha, Jeshi la Polisi limesema limeanza uchunguzi kuhusu chanzo cha tukio hilo, huku likitoa wito kwa jamii kushirikisha watu kuhusu changamoto wanazopitia ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo na si kujichukulia sheria mkononi.

Send this to a friend