Mfugaji adaiwa kumtishia kumuua Mkuu wa Wilaya

0
38

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zaynab Telack ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kumkamata na kumfikisha mahakamani mfugaji anayedaiwa kumtishia maisha Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Zainabu Kawawa ili kujibu tuhuma zinazomkabili za kumtishia kumuua kiongozi wa Serikali.

Ametoa agizo hilo baada ya Kawawa kudai kwenye kikao cha viongozi na wafugaji kuwa mmoja wa wafugaji amemtishia maisha baada ya kumhoji kama ameingiza mifugo wilayani humo kihalali.

Telack amesikitishwa na tukio hilo huku akisema kuwa haiwezekani kwa kiongozi wa Serikali aliyepewa dhamana ya kuongoza watu Kilwa kutishiwa usalama wa maisha yake huku yeye akikaa kimya bila kuchukua hatua yoyote ya kisheria.

Moshi wadaiwa kuuza nyama na supu ya mbwa

“Huyu ni kiongozi aliyepewa kazi ya kumsaidia Rais wa Tanzania kwenye wilaya, iweje anatishiwa usalama wake wa maisha tuendelee kukaa kimya, haiwezekani. Ninaagiza RPC hakikisha huyu mfugaji anakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili,” amesema.

Chanzo:Nipashe

Send this to a friend