Mfumuko wa bei Nigeria wazidi kupanda na kufikia 27.33%

0
33

Wananchi wa Nigeria wanakabiliana na changamoto kubwa kutokana na ongezeko la mfumuko wa bei, ambao umefikia asilimia 27.33 mwezi Oktoba ikilinganishwa na asilimia 26.72 mwezi Septemba. Hii inamaanisha gharama za maisha zimeongezeka, na hivyo kuleta shinikizo kubwa kwa raia wa kawaida.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na Shirika la Takwimu la Kitaifa (NBS) inaonyesha kwamba kiwango cha mfumuko wa bei mwezi Oktoba 2023 kilionyesha ongezeko la asilimia 0.61 ikilinganishwa na mwezi Septemba 2023. Kwa misingi ya mwaka hadi mwaka, kiwango cha mfumuko wa bei mwezi Oktoba 2023 kilikuwa asilimia 6.24 juu zaidi ikilinganishwa na mwezi Oktoba 2022, ambapo kilikuwa asilimia 21.09.

Utafiti: Hali ya umasikini Tanzania umepungua

Gharama za chakula pia zimepanda kwa kasi, na kiwango cha mfumuko wa bei kwa chakula kimefikia asilimia 31.52 mwezi Oktoba, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.80 ikilinganishwa na mwezi Oktoba mwaka uliopita ambapo kiwango kilikuwa asilimia 23.72.

Wakati huo huo, wananchi wa Nigeria wanaonesha kutoridhishwa na jinsi serikali inavyosimamia fedha za umma, hasa wanavyoona athari za sera kama kuondolewa kwa ruzuku kwenye mafuta na kudai kwamba matumizi ya serikali hayalingani na hali yao ya maisha inavyozidi kuwa ngumu.

Send this to a friend