Mgambo auawa kituoni akiamulia ugomvi wa wapenzi

0
34

Mgambo wa Kijiji cha Mkengwa katika kisiwa cha Kibuyi wilayani Rorya, Fred William (47) amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu shingoni alipokuwa akiamulia ugomvi wa wapenzi katika kituo cha polisi.

Tukio hilo limetokea Agosti 30, mwaka huu baada ya mgambo huyo kumzuia mwanaume huyo kuingia ndani ya kituo cha polisi kwa lengo la kumpiga mke wake aliyekimbilia kituoni hapo baada ya kutishiwa kuuliwa na mwanaume huyo.

Kwa mujibu wa mashahidi wa tukio hilo, mke na mume walifika kituoni hapo wakiwa wanakimbizana jambo lililoleta taharuki kituoni hapo, na ndipo ilimlazimu mgambo huyo kumzuia asiingie ndani.

Shahidi Nico Azaria ameeleza kuwa “baada ya mgambo kumshika mtu huyo alimng’ata bega la kulia ndipo mgambo akamuachia na kisha mtu huyo kuchomoa kisu na kumchoma mara mbili shingoni upande wa kulia.”

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkengwa, Rajabu Obure amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa wa tukio hilo anafahamika kwa jina la utani la ‘Njiwa’ mkazi wa Kyangasaga ambaye huja kijijini hapo kwa ajili ya shughuli za uvuvi na kuondoka.

Send this to a friend