Mganga alawiti watoto sita akiwapa matibabu

0
48

Mganga wa kienyeji mkazi wa Majengo ya Mpanda mkoani Katavi, Akili Abakuki maarufu kama Jimmy (38) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwalawiti watoto sita wakati akiwapatia matibabu nyumbani kwake.

Kaimu wa Jeshi la Polisi Mkoani hapo, Sylivester Ibrahim amesema mtuhumiwa alikamatwa Mei 8 mwaka huu baada ya mmoja wa wazazi wa watoto hao kugundua kuwa mwanaye mwenye umri wa miaka 10 aliyepelekwa kwa mganga huyo kutibiwa amelawitiwa.

Kamanda amebainisha kuwa, wazazi wa watoto hao wenye umri kati ya miaka 6 na 12 waliwapeleka kwa mganga huyo ambapo aliwapa masharti kuwa, tiba zake ni lazima azitoe usiku hivyo lazima watoto hao walale nyumbani kwake bila ya wazazi wao.

Wazazi wawanywesha watoto pombe wakienda vilabuni ili walale wasiwasumbue

Inadaiwa usiku mganga huyo huwarubuni kwa zawadi ndogo ndogo kama biskuti na peremende kisha kuwapaka mafuta mwili mzima na kuwaingilia kimwili.

Anasema vitendo hivyo huvifanya chumbani kwake usiku wa manane huku akiwatishia watoto hao kutowaambia wazazi wao kitendo walichofanyiwa.

Kamanda anawasihi wazazi kufuatilia vitendo wanavyoweza kuwa wamefanyiwa watoto wao na kuwahimiza waache kushikilia imani potofu za kishirikina.

Send this to a friend