Mganga mbaroni kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi akidai ni tiba

0
46

Mganga wa kienyeji, Stephano Mjema (36) mkazi wa Ndungu wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi wawili kwa nyakati tofauti wakati walipokwenda kupatiwa matibabu nyumbani kwake.

Inadaiwa mganga huyo alikuwa akiwaingilia kwa nguvu wanafunzi hao mmoja wa darasa la sita na mwingine wa darasa la saba akidai anawaingizia dawa kwa kutumia uume wake.

Hata hivyo taarifa za ukatili unaofanywa na mganga huyo ziliibuka baada ya mmoja wa wanafunzi hao kufanya jaribio la kutaka kujiua kwa sumu ya panya na baada ya kufanyiwa mahojiano polisi ndipo akaeleza kuwa amechoshwa na vitendo anavyofanyiwa na mganga huyo.

Akizungumza juu ya suala hilo, Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amewataka wazazi kuwajibika kwa watoto wao, akiongeza kuwa ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha mwanae anakuwa katika mazingira salama.

Naye mratibu wa Kitengo cha Familia na Watoto wilaya ya Same, Ally Shehonza amesema baada ya kumhoji mwanafunzi huyo amedai mara ya kwanza baba yake mzazi ndiye aliyempeleka kupata matibabu na baadaye alimuacha aende peke yake, na kadri siku zilivyokwenda mganga huyo alianza kumuingilia kwa nguvu.

Send this to a friend