Mganga wa kienyeji amng’oa mkewe meno kisa shilingi 200

0
53

Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshikilia Musa Abdallah, mkazi wa Kijiji cha Nyakatende wilayani Musoma kwa tuhuma za kumng’oa meno matatu mke wake kisa ugomvi wa shilingi 200 aliyoitumia kutoka kwenye mauzo ya mahindi kumnunulia mtoto andazi.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Salum Morcas amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni mganga wa kienyeji akisaidiana na mke wake mwingine ambaye bado hajatiwa nguvuni walimkamata mke mdogo wakamlaza chini na kisha mume wake akamng’oa meno kwa kutumia koleo ‘pliers’.

Ameongeza kuwa tukio hilo limetokea kati ya mwezi wa tatu na mwezi wa tano, na kwamba mwanamke huyo alishindwa kutoa taarifa mapema polisi kutokana na mtuhumiwa kumfungia ndani ya nyumba hadi taarifa zilipotoka kwa wasamaria wema.

Mtuhumiwa huyo anashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi ili hatua stahiki zichukuliwe ikiwemo kumfikisha mahakamani.

Send this to a friend