Mganga wa kienyeji apatikana na mafuvu 24 ya binadamu nchini Uganda

0
18

Mwanaume mmoja nchini Uganda anayetambulika kwa jina la Ddamulira Godfrey anashikiliwa na polisi baada ya kupatikana na mafuvu 24 ya vichwa vya binadamu ambavyo anadaiwa kuwa alikuwa akivitumia kwa ajili ya kafara.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Patrick Onyango, amesema mtuhumiwa huyo atashtakiwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupiga Marufuku Kafara za Binadamu na kwamba endapo atapatikana na hatia, anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha gerezani.

“Tunamshtaki chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupiga Marufuku Kafara za Binadamu, ambayo inapiga marufuku mtu kumiliki sehemu za miili ya binadamu na kafara za binadamu,” ameeleza.

Aidha, ameeleza kuwa kwenye kibanda cha mwanaume huyo anayedai kuwa ni mganga wa jadi na mtaalamu wa mitishamba, pia yalipatikana mabaki ya wanyama na ngozi, na kwamba polisi wanaendelea kuchunguza kwa matumaini ya kupata mabaki zaidi ya binadamu.

Send this to a friend