Mgodi wa North Mara kuziwezesha kampuni 15 za Kitanzania

0
41

 

Kampuni ya madini ya Barrick Gold Corporation imetangaza kuwa makampuni 15 yatahitimu kutoka kwenye progamu ya kuendeleza biashara za ndani.

Programu hiyo imekuwa ikitoa mafunzo ya kitaalam na ushauri wa kibiashara kwa makampuni madogo na ya kati ili kuziimarisha kiujuzi na kuziwezesha kunufaika na mnyororo wa thamani wa sekta ya madini.

“Tunajivunia kwa kuongoza njia kwa kufanikiwa kuendesha program hii ya maendeleo ya biashara za ndani ya nchi na tumetimiza wajibu zaidi ya sheria zilizopo maudhui ya ndani. Maudhui ya ndani ni muhimu kwa shughuli zetu na tunapoziimarisha kampuni ndogo na za kati, tunaziimarisha na jamii zinazotuzunguka,” Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Barrick, Mark Bristow amesema.

Janeth Reuben Lekashingo, Kamishna wa Kamisheni ya Madini amesema: Serikali kupitia Kanuni za Maudhui ya Ndani ya Mwaka 2017 imetoa mfumo wezeshi kwa ajili ya biashara za ndani ili zinufaike kutoka kwenye uwekezaji unaofanywa nchini kupitia fursa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani.

Tangu kuanzishwa kwa programu hiyo mwezi Novemba mwaka 2021, makampuni ya ndani ya nchi yamepatiwa mafunzo mara nne kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi minne kwa lengo la kujenga uwezo na kusaidia makampuni yaweze kunufaika na fursa zilizopo kwenye sekta ya madini.

Send this to a friend